April 2, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Pacha Milionea waja na truck mpya “Nyumbani”

Na Mwandishi wetu ,Timesmajira

WASANII wa Kitanzania waishio nchini Marekani wanaotambulika kwa jina la Pacha Milionea wameachia truck mpya ya nyimbo ya Singeli inayoenda kwa jina la Nyumbani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasanii hao ambao ni mapacha,walisema wamesema wameachia truck yao hiyo rasmi kutokana mziki wa singeli kuja kwa kasi na kufanya vizuri zaidi nchini Tanzania.

Mmoja wa wanamziki hao, Eliya Kimanga amesema truck hiyo inawatambulisha kama wao Watanzania na wanakila aina ya kujivunia na miondoko ya nyimbo za mziki wa singeli.

“Tutahakikisha mziki huu unafika mbali zaidi na unakuwa wa kimataifa zaidi na kuwa na radha zaidi kimziki hivyo tutahakikisha mziki huu unakuwa na mvuto kwa wasikilizaji mbalimbali wa mziki,”amesema.

Aidha kwa upande wa Msanii Elisha Kimanga amesema awali walipokuwa nchini Tanzania wakikuwa wachezaji (Dancer)kupitia Tanzania House of Talent (THT) ambapo walifanya kazi na wasanii mbalimbali akiwemo Snura,Baba Levo,Msami na Diamondi Platinum.

“Kupitia THT kushirikiana na wasanii hao tulijikuta tunapenda mziki na kuanza kuimba na watu walianza kutukubali huku baadhi ya wasanii tulikuwa tunaimba nao live nao walitukubali sana.

“Hapo ndo safari ya mziki yetu ilipoanzia ilikuwa maeneo ya Tandale ambapo tuliachia nyimbo yetu ya kwanza inayotambulika kwa jina la Zuzu mwaka 2021,”amesema.

Amesema walipotoa nyimbo hiyo walisafiri na kwenda Marekani mji wa Boston na kuendelea na harakati zao ambapo walipata kufanya Show kubwa na wasanii wa Tanzania wakiwa wanaenda huko.

Amesema tayari walifanya nyimbo kwa kushirikiana na Country Boy na Mr Blue ambapo sasa wamefungua studio yao inayoitwa Tam kama Banana ili kuendelea kufanya mziki mzuri .

“Tumekuwa tunafanya vizuri sana katika kiwanda cha mziki na wasanii mbalimbali wakija nchini Marekani uwa tunashirikiana nao katika show zao mbalimbali, “amesema Martin.