January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Othman akutana na viongozi ngazi mbalimbali wa Act -Wazalendo Unguja

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, leo Jumapili Mei 19, 2024 amehudhuria, akiwa Mgeni Rasmi, katika Kikao cha Viongozi wa Kamati za Uongozi za Mikoa, Majimbo, Matawi, pamoja na Ngome zake, kutoka Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, ambao umejumuisha Mikoa ya kichama ya Magharibi ‘A’, Magharibi ‘B’, na Mjini Unguja.

Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Viongozi wa Ngazi mbalimbali wa Chama hicho, wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa; Naibu Katibu Mkuu Mstaafu na Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui; na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Mansour Yusuf Himid, kimefanyika huko katika Ukumbi wa Majid Kiembe-samaki, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja.

Kikao hicho ni Mwendelezo wa Vikao vya Shukurani kwa Wanachama sambamba na Uimarishaji wa Chama hicho, tangu walipokamilisha Uchaguzi wa Ndani, mapema Machi 2024, na vimekuwa vikifanyika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.