January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Othaman amjulia hali Mwakilishi Mstaafu wa Jimbo la Uzini

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, leo Februari 19, 2023 amefika na kumjulia hali Mwakilishi Mstaafu wa Jimbo la Uzini – Unguja, Mohammed Raza Hassanali, huko Nyumbani kwake, Ali Abass Tower, Jengo lililopo katika Mtaa wa Hazrat Abass, Kata ya Kisutu, Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Othman ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, baadhi ya Watendaji na Maafisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.