January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

OSHA,yawanoa wahandisi wanawake

Na Bakari Lulela, Timesmajira, Online

WAKALA wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA),limetoa elimu kwa Wahandisi wanawake, kufahamu umuhimu wa ushirikishwaji,katika maendeleo ya uchumi wa nchi

OSHA pia,imewakumbusha Wahandisi Wanawake,kutambua kuwa suala la afya na usalama ni jambo muhimu.

Akizungumza jijini Dar-es-Salaam, Agosti 21,2024,Ofisa Mafunzo wa OSHA,Simon Lwaho amesema,Wahandisi ndio waendeshaji wa mitambo, viwanda , migodi pamoja kusanifu majengo mbalimbali,hivyo suala la usalama na afya kwao ni jambo la msingi sana.

Lwaho, amesema,moja ya jukumu la OSHA ni kutoa elimu na kuwakumbusha wadau kujizuia na vihatarishi mbalimbali vilivyopo maeneo yao ya kazi.