September 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

OSHA: Mkaa huondoa sumu ya pombe mwilini

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)imesema Mkaa
uondoa sumu ya kukata pombe mwilini kwa walevi.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Huduma ya kwanza wa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA)Moteswa Meda, wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Tanzania (JOWUTA)mafunzo yaliofunguliwa na Mtendaji mkuu wa OSHA ,Hadija Mwenda, makao ,makuu ya OSHA.

Moteswa Meda alisema mkaa ni kitu muhimu kukaa nacho nyumbani kwa kuwa kina msaada mkubwa kwa Binadamu hasa katika eneo la uokozi.

“Mkaa uondoa sumu ya pombe Mwilini kwa walevi. Mkaa unaweza kuokoa maisha ya mtu aliyekunywa sumu kama mtu amekunywa sumu ya aina yoyote au idadi kubwa ya vidonge ambapo kinachofanywa sio kumpa maziwa au maji badala yake ni kumpa mkaa atafune kama anaweza kutafuna ” alisema Meda.

Alisema mtu anapokunywa sumu au kilevi apondewe mkaa hadi uwe na unga kumeza bila maji mtu aliyekunywa sumu aina yoyote au vidonge anatakiwa asipewe Kimiminika akipewa anaongezewa uharaka wa kufa maana anaenda kuipa nguvu sumu isambae kwa haraka Mwilini.

Aidha alisema Kama mtu awezi kutafuna mkaa apondewe uwe unga ili kumuwezesha bila maji ambapo baadhi ya waandishi wa habari wa Tanzania wa chama cha JOWUTA walipatiwa mafunzo na OSHA kwa ajili ya elimu hiyo wakaitoe kwa umma kwani jamii nyingi awajui mkaa kama ni tiba ya kuokoa uhai wa mtu.

“Mkaa ukiingia tumboni kwa wingi unakwenda kuifonza ile sumu iliyopo mwilini na kumpunguzia mtu hatari ya kufa ,hata hivyo pamoja na kutoa huduma hiyo ya kwanza na kuakikisha aliyekunywa sumu anakimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi ” alisema.

Alisema kwa mtu aliyelewa kwa kiwango kikubwa anaweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida kwa muda mfupi sana endapo atatafuna mkaa unafanya kazi kwenye kuondoa sumu kiwango cha pombe mwilini.

Alisema mkaa pia wa kawaida unatumiwa majumbani kwa shughuli za kijamii ikiwemo kupikia na kazi nyingine kutumika katika huduma za kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu au kulewa.

Mwenyekiti wa JOWUTA Muusa Juma, alisema OSHA ni Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi ni Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya afya ya mwaka 2003 ikiwa na lengo la kuweka viwango vya usimamizi wafanyakazi wawapo kazini.

Mtendaji mkuu wa OSHA Hadija Mwenda, alisema wameona umuhimu wa kuwapa elimu waandishi wa habari wa JOWUTA kutokana na jitihada zao kubwa na nafasi kubwa walionayo ya kuwasiliana na jamii kwa haraka.