TOKYO, Japan
NYOTA nambari mbili kwa ubora duniani katika mchezo wa tenis upande wa wanawake Naomi Osaka amesema, anataka kuwa katika kiwango cha juu kwenye mashindano ya Olimpiki, baada ya kujiondoa kwenye mashindano kadhaa.
Osaka, mwenye umri wa miaka 23 raia wa Japan, alimwambia mtangazaji wa kimataifa wa Japani NHK kuwa, anajiandaa kucheza kwenye uwanja wa nyumbani Tokyo katika mashindano ya Olimpiki ambayo yaliahirishwa, kutokaa na Ugonjwa wa Corona.
“Ninajiandaa na mashindano ya Ollmpiki ili niweze kufanya vyema. Tangu kupata umakini wa ulimwengu, siku zote nimekuwa na wasiwasi. Hii ni hali inayoongoza kwa mashindano makubwa,” amesema Osaka.
Osaka alianzisha mjadala juu ya afya ya akili baada ya kuacha kampeni yake ya French Open mechi moja tu juu ya mzozo wa majukumu ya media.
Mchezaji huyo wa Kijapani amesema mikutano ya habari baada ya mechi ilikuwa mbaya kwa afya yake ya akili, hivyo alihitaji muda ili aweze kupata nafuu.
Hata hivyo, alitozwa faini ya dola 15,000 na kutishiwa kutostahiki kutoka kwa Roland Garros baada ya kukataa kutekeleza ahadi za lazima za media.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania