Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Muheza
KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imemueleza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan jitihada mbalimbali ambazo imekuwa ikizifanya katika kuunga mkono kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.

Akizungumza mbele ya Rais Samia
baada ya kutembelea banda la Oryx wakati wa uzinduzi wa kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kitaifa iliyozinduliwa uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza mkoani Tanga, ,Meneja Miradi ya Nishati safi kutoka Oryx Gas Peter Ndomba, amesema katika kufanikisha kampeni ya matumizi ya nishati safi kampuni hiyo imefanikiwa kushiriki kwa vitendo.
“Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa ajenda yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Oryx Gas tumekuwa wadau na tumefanya jitihada tangu ilipotangazwa kama ajenda rasmi ya nchi kwamba wananchi tuanze kutumia nishati safi ya kupikia,”.
Amesema wameongeza miundombinu ya kusambaza mitungi ya Oryx Gas hasa katika maeneo ya vijiji,ambapo kwa sasa huwezi kuikosa.
“Mitungi ya Oryx inapatikana kila miji,Wilaya na vijijini tupo .Pia tumekuwa tukishiriki katika shughuli za mbalimbali za kuwezesha ukuaji wa matumizi ya nishati safi ambapo tumeweza kuisaidia jamii mbalimbali ikiwemo ya Wanawake kwa kuiwezesha kufikia malengo hayo,”amesema.

More Stories
Rais Samia ataka mto Zigi ulindwe miradi ya maji iwe endelevu
Uwekezaji uliofanyika serikali awamu ya sita umezalisha ajira 523,891 nchini
Dkt. Matarajio: Tunataka Nishati ya Petroli iwe injini ya maendeleo