January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

OktobaFest tamasha la tamaduni za kitanzania

Kutoka kushoto, Wankyo Marando- Meneja wa chapa – Bia shirikishi (Guinness & Pilsner). Rhona Namanya- Mkuu wa Bia. Anitha Msangi Rwehumbiza- Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu. Rispa Hatibu- Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Serengeti Breweries Limited wiki hii katika uzinduzi Oktobafest kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

KAMPUNI ya bia ya Serengeti (SBL) ina furaha kutangaza OktobaFest, inayolenga kusherehekea tamaduni za kitanzania yaliyopangwa kufanyika tarehe 21 Oktoba 2023. OktobaFest 2023 inatarajiwa kuwa tukio la pekee ambalo linaunganisha watu mbalimbali ili kufurahia ladha, sauti na tamaduni za kipekee za Tanzania.

OktobaFest Tanzania ni shereheya kiepekee inayojumlisha vyakula, muziki na utamaduni wa Kitanzania. Watu wanaweza kutarajia nakshi za kipekee kupitia ladha ya vyakula tofauti na vibanda vingi vya vyakula vitavyohudumia vyakula vitamu vinavyoakisi ladha mbalimbali za kitanzania. Kuanzia vyakula vitamu vya kitamaduni hadi ubunifu wa kisasa wa mchanganyiko, OktobaFest ni tukio pekee la kitamaduni.

Safu ya muziki wa tamasha hili ni mchanganyiko wa midundo ya kitamaduni na midundo ya kisasa, inayoshirikisha wasanii wa aina mbalimbali nchini Tanzania. Wasanii hawa watapanda jukwaani ili kuonyesha sauti zao za kipekee, kuonyesha uzoefu wa muziki usiosahaulika kwa wahudhuriaji. Pamoja na hayo, muziki, maonyesho ya dansi, sanaa na mitindo yataangazia urithi wa kitamaduni wa Tanzania, na kutoa uzoefu wa kusherekea utofauti wa kanda.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti alisema kuwa, “OktobaFest sio tu sherehe ya utamaduni, lakini inalenga kuleta matokeo chanya katika sehemu zote muhimu ya jamii yetu. Serengeti Breweries imejitoa kwa dhati kuleta matokeo chanya kwa jamii inayohudumia. Tamasha hili litawasaidia wajasiriamali na wasanii kupata ustawi katika nyanja zao zinazokuza za ujasiriamali, ubunifu na uendelevu”.

Kama wadhamini wa tamasha hilo, Serengeti Breweries ina nia kuhamasisha utamaduni wa mtanzania. Kutoka chakula, mitindo na sanaa, OktobaFest inalenga wasanii wachanga kwa kutoa jukwaa kwa vipaji vinavyoibuka ili kuonyesha ubunifu wao na ustadi wa mapishi, kukuza ujasiriamali na ubunifu. Pamoja na haya, tamasha hili litajumuisha michezo mbalimbali inayounganisha teknolojia na mila, kutoa mtazamo wa pekee juu ya utamaduni wa kitanzania.

Zaidi ya hayo, OktobaFest ya SBL inachukua hatua muhimu ili kupunguza athari kwenye mazingira. Juhudi kama vile udhibiti na utupaji ovyo wa taka na mbinu endelevu zitawekwa ili kuhakikisha usafi wa mazingira katika tamasha hili.