July 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ofisi ya Waziri Mkuu yahakikisha inaendelea kuwafikia wananchi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imejipanga kuhakikisha inaendelea kuwafikia wananchi wanaopata huduma katika banda jumuishi la ofisi hiyo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa kuhakikisha wanapewa elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu ofisi hiyo pamoja na taasisi zilizochini yake.

Ameyasema hayo tarehe 04 Julai, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ikiwemo la Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Fedha na taasisi zake, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Kampuni ya simu ya halotel pamoja na Shirika la posta.

Aidha, Dkt. Yonazi ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kutembelea banda hilo na kupongeza namna watumishi wa ofisi hiyo wanavyoendelea huwahudumia wananchi na wadau wanaofika huku akiwasii watumishi hao kuendelea kuzingatia weledi zaidi katika utoaji huduma na elimu kwa umma.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya uratibu pamoja na huduma zinazotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu hivyo wananchi na wadau mbalimbali wayatumie maonesho hayo kama fursa yakujifunza kuongeza uelewa” alisema Dkt. Yonazi

Maonesho hayo ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji,”.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza jambo na wataalam kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (TIA) alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba tarehe 04 Julai, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na baadhi ya watendaji TSN alipowatembelea katika banda lao wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba tarehe 04 Julai, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia kipeperushi alipotembelea banda la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba tarehe 04 Julai, 2024.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino na Uhusiano kwa Umma TCRA Bw. Rolf Kibaja alipotembelea katika banda la ofisi hiyo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino na Uhusiano kwa Umma TCRA Bw. Rolf Kibaja alipotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akimsikiliza Meneja wa banda la Posta Bw. Khamis Swedi wakati alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba tarehe 04 Julai, 2024

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiweka saini katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo cha Mipango Vijijini wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba tarehe 04 Julai, 2024, kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti, Chuo cha Mipango Dodoma Profesa Provident Dimoso.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akimsikiliza Mratibu Msaidizi Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Aarnold Mkude alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipokea kipeperushi kutoka Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasilaino Halotel Bi. Roxana Kadio alipotembelea banda la kampuni hiyo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasilaino na Masoko Chuo cha TIA Bi. Lilian Rugaitika alipotembelea banda Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)