December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ofisi ya Msajili wataka maelezo ya Act-Wazalendo

Na Mwandishi wetu

CHAMA cha Act-Wazalendo kimetakiwa kuwasilisha maelezo kwa Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini kuhusu suala la Balozi wa Uingereza nchini Tanzania kuwasaidia katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2020 ili ishinde dhidi ya vyama vingine.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo, Kaimu Msajili wa Vyama vya siasa nchini, Sisty Nyahoza amesema chama hicho kinatakiwa kuwasilisha taarifa hiyo ili waweze kujua ukweli kuhusu taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari.

Amesema, maelezo hayo yanapaswa kuwasilishwa katika Ofisi ya Msajili siyo zaidi ya Juni 19 mwaka huu saa tisa na nusu mchana.

Ofisi hiyo ya msajili imepata taarifa kutoka katika vyombo vya habari leo Juni 12 mwaka huu ikiwemo katika Gazeti la Jamvi la Habari toleo namba 1031.

Amesema, kati ya Juni 8 na 12, kiongozi mkuu wa chama hicho cha Act-Wazalendo, Zitto Kabwe kufanya kikao na Balozi wa uingereza nchini nyumbani kwake Oysterbay Dar es Salaam.