Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (WAMM), Zanzibar imetiliana Saini ya Makubaliano (MoU) na  Kampuni ya ASER kutoka Uturuki kwa ajili ya Mradi wa ujenzi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar (Housing Development Projects in Zanzibar).Â
Hafla hiyo ya utiaje Saini ya Makubaliano imefanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Maisara, Unguja baina ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Mngereza Mzee Miraji na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo bw. Ertan
Dkt Mngereza alisema lengo la makubaliano hayo baina ya pande mbili hizo ni kuanzisha mahusiano ya kikazi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maendeleo na za biashara kwa mkopo nafuu.
Alifahamisha kwamba mradi huo unatarajiwa baada ya taratibu zote za makubaliano kukamilika kwa pande zote mbili wizara ya Ardhi na Kampuni ya ASER ikiwemo, mapendekezo ya Mradi wa nyumba na gharama zake, taratibu za kisheria, kulipa fidia, nk.
Alisema Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi inatarajia kuwa na Mradi mpya wa nyumba za Maendeleo Chumbuni Zanzibar ambapo mradi huo utajenga nyumba 1000 lakini nyumba hizo zitajengwa kwa awamu hivyo awamu ya kwanza zitajengwa nyumba 500 na awamu ya pili nyumba 500 ili kukamilisha idadi hiyo.
Pia alisema Mradi huo utajenga nyumba za vila 50 eneo la Fumba huku maeneo ya Mombasa kwa Mchina Mradi utajenga nyumba 48 za gorofa(48 flats) na nyumba za Mji Mkongwe zitafanyiwa matengenezo/ukarabati.
Mapema Naibu Waziri Wizara hiyo Juma Makungu Juma alisema Zanzibar kunamahitaji makubwa ya nyumba hivyo Kampuni hiyo imeahidi kujenga nyumba hizo mara baada ya kukamilisha taratibu zote zinazohitajika.
Alisema ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kujengwa katika maeneo tofauti Unguja na Pemba ambapo utazingatia kipato cha kila mwananchi ili kuweza kuzimudu kwa lengo la kuboresha maakaazi bora.
Aidha alifahamisha lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ( SMZ) ni kuwapatia makaazi bora wananchi wake kutokana na uchache wa nyumba zilizopo  hazikidhi mahitaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Shirika la Nyumba Zanzibar Mwanaisha Ali Saidi alisema Shirika la Nyumba Zanzibar limekabiliwa na changamoto ya kuwa na nyumba chache huku baadhi ya nyumba kua chakavu na zinahitajiÂ
Alifafanua kwamba ujio wa kampuni hiyo ya Ertan umeleta faraja kwani baada ya kukamilika kwa Mradi huo Shirika la Nyumba Zanzibar litaweza kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
 Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya ASER bw. Ertan Murat ameishukuru Serikali ya Mapniduzi Zanzibar na Wizara ya Ardhi kwa kuichagua kampuni yake kufanyakazi nao, hivyo ameahidi atafanyakazi hiyo kwa uaminifu na kwa viwango vilivyohitaji katika ujenzi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja