Na Stephen Noel,TimesMajira Online, Mpwapwa
SHULE ya Msingi Idilo iliyoko Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma nusu ya wanafunzi wote wamekuwa wakisoma huku wamekaa chini kwenye vumbi kutokana na shule hiyo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati.
Akizungumza na TimesMajira, Mkuu wa shule hiyo, Jonson Charles amesema madarasa matatu kuanzia la tano, la tatu na la nne wamekuwa wakisoma huku wakiwa wamekaa chini na kuathiri ujifunzaji kwa watoto hao.
Charles amesema, kwa sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 415 ikiwemo wavulana 208 na wasichana 207 na bado wanaendelea na uandikishaji na wana madawati 50 na upungufu ni madawati 93. Kwa kina soma Gazeti la MAJIRA la Januari 25, 2021.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea