Na David John TimesMajira Online, Njombe
MKURUGENZI wa Usalama chakula kutoka wizara ya kilimo Dkt. Honest Kessy, ameutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii nchini NSSF kwenda vijijini kwa wakulima ili kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.
Kessy amesema, kuna changamoto ya wakulima hususani vijijini kutoelewa umuhimu wa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, nijukumu la mifuko hiyo kuwafikia walipo na kuwapa elimu ya kuona umuhimu wa mifuko hiyo.
Kessy ameyasema haya leo, baada ya kutembelea banda la NSSF kwenye viwanja vya mji Mwema njombe katika siku ya chakula duniani ambayo yanakwenda sambamba na maadhimisho ya chakula na lisha ambayo inabeba kauli mbiu ya ‘Kesho njema inajengwa ma lishe bora endelevu’.
“NSSF mnafanya kazi nzuri sana lakini nawashauri kuingia huko vijijini wakulima waliko ili kuwapa elimu zaidi ya umuhimu wa kujiunga na mifuko hii maana kuna wengine hawajui umuhimu wa mifuko hii,”amesema Honest.
Naye Meneja wa NSSF mkoa wa Njombe Mrisho Mwisimba, amewataka wakulima mkoani humo kufika katika maonyesho hayo na kutembelea kwenye banda la NSSF, ili kupata elimu kuhusu Mfuko huo.
Mwisimba amesema, wao Kama NSSF wapo kwa ajili ya wananachi pamoja na wakulima hivyo wafike kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ili kupewa elimu zaidi ambayo itawasaidia kujiunga katika mfuko.
“Ndugu mgeni rasmi tupo hapa kwa ajili ya kuwapa elimu wakulima ikiwa pamoja na kuwataka wajiandikishe kwenye Mfuko wa Jamii na kubwa watapata mafao ya uzeeni na utoaji wa mikopo,” amesema
NSSF wapo mkoani hapo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani humo na yapo chini ya wizara ya kilimo.
%%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Kishindo Mkutano wa Nishati leo, kesho Dar
Puma Energy Tanzania yampongeza Rais Samia kwa mazingira mazuri ya uwekezaji, yang’ara tuzo za TRA
CHAMUITA wamtunuku Tuzo Msama