January 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mohamed Noray

Noray ahimiza wananchi kumchagua Magufuli

Na Esther Clavery, TimesMajira Online, TUDACo

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Noray amewasihi wananchi kumchagua tena mgombea Urais wa chama hicho, Dkt. John Magufuli ili aweze kuleta maendeleo zaidi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Pia amesema Dkt. Magufuli, anastahili kuendelea kuogoza zaidi ya miaka 20 kwani ni kiongozi wa kuigwa duniani kote.

Noray ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni za CCM kwa Mkoa wa Dar es Salaam, uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Amesema, katika miaka mitano aliyoiogoza Dkt. Magufuli, ameweza kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kubadilisha mfumo mzima wa serikali pamoja na kuwakwamua wanyoge.

“Tumchangue mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi, aweze kuogoza miaka mitano mingine. Rais Magufuli katika uogozi wake amefanya mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo mizuri ya uongozi,” amesema.

Noray amesema, katika uongozi wake wa kipindi cha miaka mitano amefanikiwa kujenga viwanja vya michezo katika kila mkoa, madaraja, viwanja vya ndege, Reli ya mwendo kasi, Bwal kufua umeme kutok mto Rufiji na kuweka mifumo mizuri katika uongozi.

Amesema, mgombea huyo ni kiongozi ambaye amekuwa akifuata nyayo za viongozi waliowahi kuongoza Tanzania.

“Rais Magufuli ni kiongozi ambaye amekuwa akifuata nyayo za viongozi waliowahi kuogoza, akiwemo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Hayati Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi na Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, “amesisitiza Norya.

Amesema Nyerere anakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya katika kulifikisha taifa la Tanzania hapa lilipo.

“Baba wa Taifa amefanya mambo mengi katika taifa hili, ametukomboa katika ukoloni mamboleo. Pia nimekuwa mtu wa karibu na familia hii kwani niliwahi kusoma na mwanaye, Madaraka Nyerere katika Shule ya Sekondari Tambaza,” amesema Noray.

Amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 mwaka huu, kuhakikisha wanapiga kura kumchagua Dkt. Magufuli aongoze kwa miaka mitano mingine aweze kumaliza aliyoyaanzisha.

%%%%%%%%%%%%%%%%%