December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nomcebo Zikode mbioni kutinga mahakamani

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MWIMBAJI wa Wimbo wa ‘Jerusalema’, Nomcebo Zikode

amedai, anajipanga kwenda mahakamani kudai haki yake kwa

kuwa tangu wimbo huo uliojiozolea umaarufu duniani toka

mwaka jana, hajawahi kulipwa chochote.

Akizungumzia hilo kupitia kwenye ukurasa wake wa

instagram amedai,hajawahi kulipwa hata senti moja wakati

Master KG na lebo ya Open Mic wakijizolea mabilioni.

Nomcebo ambaye alishirikiana na Master KG katika wimbo

huo wenye watazamaji milioni 421 kwenye mtandao wa

Youtube, amesema Mbali na sauti yake kwenye jerusalema,

pia aliandika wimbo huo pamoja na Master KG.

“Asante kwa mashabiki wote wa Jerusalema mmefanya ndoto

zangu kuwa za kweli, kwa kupata wimbo maarufu

ulimwenguni. Sauti yangu na mashairi yamepita

ulimwenguni, lakini bado.

“Upendo na msaada kutoka kwa mashabiki wa Jerusalema

umekuwa nguvu yangu hasa wakati huu mgumu. Mimi kama

msanii wa kike, siwezi kukaa kimya tena juu ya hili,

suala sasa liko kwa mawakili wangu,” amesema Nomcebo.