Na Angela Mazula, TimesMajira Online
BENKI ya NMB Makao Makuu hapa nchini imewapokea rasmi wafanyakazi wote wa iliyokuwa benki ya kibiashara China nchini Tanzania ambao benki kuu imehamishia mali na madeni yote ya benki hiyo kwenda NMB.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwapokea wafanyakazi hao 12, kutoka benki ya kibiashara ya China Nchini ambao kwa sasa wanakuwa wafanyakazi rasmi wa benki ya NMB,
Afisa mtendaji mkuu wa benki ya NMB Ruth Zaipuna, amewakaribisha na kuwataka kuungana na wafanyakazi wa benki hiyo katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa na benki yanafanikiwa.
Aidha, Zaipuna amewahakikishia wafanyakazi hao kuwa watapewa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha wanaendana na tamaduni za benki ya NMB ambayo inawateja zaidi ya million nne ndani na nje ya nchi na inamilikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilmia 31.8.
Akiongea kwa niaba ya wafanyakazi wengine, mmoja wa wafanya kazi hao kutoka benki ya kibiashara ya China, Phales Kiwanga ameushukuru uongozi wa NMB kwa kuwaamini na kuweza kuwachukua ili waongeze nguvu katika benki hiyo ili kuleta mafanikio zaidi, na kuahidi kuwa watatumia uzoefu waliokuwa nao kutoka ili kuleta tija zaidi katika ufanisi wa kibenki.
Benki ya NMB, ambayo hadi sasa inajumla ya wafanyakazi 3400, matawi 227 katika sehemu mbalimbali nchini, Mashine za kutolea fedha ATM 700 na mawakala 8000.
Hata hivyo mwezi March mwaka huu, benki kuu ya Tanzania ilichukua uamuzi wa kuhamishia mali na madeni yote ya iliyokuwa benki ya biashara ya China Kuja Benki ya NMB, benki ambayo inaongoza kwa ukubwa nchini, inaongoza kwa mtandao, mizania na kwa mtandao wa matawi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa