March 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yawapa tabasamu wanafunzi wa kike Sekondari ya Usongwe

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya 

BENKI ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu imetoa msaada wa bati 120 zenye thamani ya Mil. 5 kwa  ajili ya ujenzi wa Bweni la watoto wa kike  shule ya Sekondari Usongwe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya katika kuunga mkono serikali ya awamu ya sita upatikanaji wa huduma bora za elimu hapa nchini.

Mbali ya kukabidhi bati hizo pia Benki  hiyo   imekabidhi kompyuta tano  za kujifunzia kwa shule  ya Sekondari Iziwa iliyopo halmashauri ya Jiji la Mbeya,

Akizungumza  Machi 20,2025 wakati wa kukabidhi msaada huo wa bati kwa shule ya Sekondari Usongwe pamoja na Kompyuta tano za shule ya Sekondari Iziwa

 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya  Nyanda za  juu,Wogofya Mfalamagoha amesema kuwa changamoto za sekta ya elimu Tanzania kwa Benki ya NMB ni jambo la kipaumbele na kuwa kutokana na ukweli kwamba elimu ndio  kipaumbele kikuu kwa maendeleo  

Mfalamagoha amesema kuwa  benki hiyo inatambua serikali ya awamu ya sita chini ya  Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia elimu Bora kwa nguvu zote katika kuboresha mazingira ya utoaji elimu mjini na Vijijini 

Tulipopata maombi ya kuchangia maendeleo ya elimu katika Shule hizi tuliamua mara moja kuja kushirikiana nanyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya sekta hii muhimu kwa jamii yetu  kama Benki ya NMB tunao wajibu wa  kuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na  faida tunayopata amesema Meneja huyo wa Kanda 

Aidha  Mfalamagoha amesema benki hiyo  kwa miaka mingi pia imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye elimu ikiwemo madawati vifaa vya kuezeka,vitanda,magodoro na vifaa vingine vya kusaidia matibabu, na majanga yanayoipata nchi 

Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Mohamed Fakil ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Mbeya amesema kuwa  benki ya NMB ni wadau wakubwa na kusema serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu   kusema wadau wapo kwa ajili ya kusaidia na kuchochea maendeleo kwenye maeneo ambayo serikali kwa upande wake imeshindwa kukamilisha ndo sababu matatizo yapo na yakiisha hakutakuwa na sababu ya kuongeza kuendelea kutoa msaada.

“Mwaka jana tulitangaza madarasa kukamilika lakini baada ya kutangaza kukamilika lakini wanafunzi wa kidato cha kwanza wameongezeka mara mbili yake maana yake ni lazima madarasa yaongozek ndo maana watumishi wameendelea kuajiliwa ili watatue matatizo yaliyopo kwa hiyo sisi tunategemea leo mmeleta bati kesho mtakuja kukarabati ukumbi wetu huu tuliokaa haufanani na hadhi ya shule ambayo haitoi ufaulu mbaya 

Mkuu wa shule ya Sekondari Usongwe,Mwl. Varelia Mtega amesema kuwa wamepokea bati bando 11 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wa kike ambayo ilikuwa ahadi ya Benki ya NMB katika mahafali ya kidato cha sita may Mwaka jana.

Ofisa Elimu wilaya ya Mbeya Aliko Mbuba amesema kuwa Misaada inayotolewa na Benki ya NMB kitaaluma wanaendaelea kuboresha elimu Usongwe na kwamba kwa mkoa wa Mbeya Usongwe Sekondari ndo shule inayofanya vizuri .