Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online,Tanga
BENKI ya NMB imeshiriki kwenye maadhimisho ya elimu,ujuzi na ubunifu yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya sekondari Popatlaly huku wakitoa fursa kwa vijana wenye bunifu mbalimbali kwenda kufanya majaribio kwenye benki hiyo.
Hayo yalisemwa leo na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo huku mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda ambapo amesema kwamba benki hiyo inatambua umuhimu wa ubunifu katika maendeleo ya nchi.
Amesema kwamba wao kama benki pamoja na mfadhili wanatoa Jukwaa Maalumu (Platform) kuwakaribisha vijana kufanya ubunifu,maendeleo ya kibunifu na miradi hiyo wamekuwa wakiifadhili.
Hata hivyo amesema kwamba benki hiyo pia inasaidia kuendelea kuleta chachu ya maendeleo ya ubunifu Tanzania hivyo wataendelea kuwaunga mkono kuhakikisha sekta hiyo inapiga hatua.
“Ninawakaribisha vijana wenye bunifu mbalimbali waje kufanya majaribio yao kwenye benki yetu tuna platform NMB Sign Box nzuri inatoa nafasi ya bunifu tupo tayari kushirikiana nao kama Wizara kuhakikisha ubunifu unaleta chachu ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini,”amesema.
Akizungumza wakati akifungua maadhimisho hayo Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali ipo katika mchakato wa kujenga shule 100 za mafunzo ya amali nyanja ya ufundi nchi nzima ili kuwawezesha vijana wa kitanzania kuweza kujiajiri au kuajiriwa kupitia ujuzi watakaopata kupitia vyuo hivyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Pastrobas Katambi amesema dunia ya sasa ina mabadiliko makubwa hasa kwenye masuala ya sayansi na teknolojia, ujuzi na ubunifu hivyo ni wakati wa vijana wa kitanzania kwenda sambamba na mabadiliko hayo.
Awali Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amesema wanafunzi 27 walishinda shindano la ujuzi na ubunifu ngazi ya vyuo ambao watafanyiwa mchakato na kupatikana wanafunzi 3 wa fani tofauti ambao watakwenda kushiriki mashindano ya kikanda na kimataifa mapema mwaka 2025.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â