November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yashinda Tuzo 5 za Kimataifa, yatajwa Benki Bora Tanzania 2024

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

Benki ya NMB imepokea Tuzo 5 za kimataifa ambazo kwa ujumla wake zinaitambua NMB kama benki kiongozi nchini katika biashara, utoaji huduma za kidijitali, kufuata misingi ya utawala bora na uzingatiaji wa maslahi ya jamii katika shughuli zake.

Tuzo hizo – zilizotolewa na Jarida la Kimataifa la Euro Money katika hafla iliyofanyika jijini London, Uingereza tarehe 18 Julai 2024 – ni pamoja na:

➡️ Benki Bora Tanzania (Kwa mara ya 11 ndani ya miaka 12)

➡️ Benki Bora ya Kidijitali Tanzania

➡️ Benki Bora inayofuata misingi imara ya Utawala Bora, Ustawishaji wa Jamii na Utunzaji Mazingira (ESG) Tanzania.

➡️ Benki Bora ya Wateja Maalum Tanzania

➡️ Benki Bora ya Wateja Wenye Uwezo Mkubwa wa Kifedha Tanzania (High Net Worth Individuals)

Tuzo hizi zimepokelewa na Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB – Alfred Shao aliyeambatana na Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya Wawekezaji, Edgar Ndani na Afisa Uhusiano, Bethuel Kinyori.

“Tuzo hizi ni matokeo ya ufanisi wa kiutendaji kwa ujumla, mkakati wa matumizi ya njia za kidijitali, huduma jumuishi za fedha na uendeshaji wa biashara inayomgusa kila Mtanzania,” alisema Bw. Shao.

“Tunawashukuru Watanzania, wateja wetu ,wadau na wafanyakazi wetu wote kwa ujumla kwa kuendelea kutuamini na kutufanya washirika katika kukuza shughuli zenu kupitia masuluhisho yetu bunifu,” alisema Bw. Shao.