Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya
BENKI ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu kusini imekabidhi msaada wa vitanda na magodoro vyeye thamani ya zaidi ya Mil.9 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ili kuwezesha wagonjwa kulala katika eneo salama.
Msaada huo uliokabidhiwa ni pamoja na mashuka 20 na vitanda 20 huku fedha zilizo tumika ni sehemu ya asilimia moja ya faida yake.
Msaada huo umekabidhiwa Agosti 21,2025 na Kaimu Meneja wa Benki hiyo, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Lembris Israel kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa katika hafla fupi iliyofanyika katika Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.

“Tunao wajibu wa kuhakikisha jamii inafaidika na faida tunayoipata kupitia mfuko wa kusaidia jamii kwa kuthibitisha NMB imejikita zaidi kutatua changamoto katika maeneo ya elimu,afya na misaada ya hali na mali katika nyakati ngumu kama za majanga “amesema Kaimu Meneja huyo.
Aidha amesema kuwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 mfululizo wamekuwa wakitenga maeneo yenye makundi.
Aidha Israell amesema kuwa kupitia mfuko wa kusaidia jamii kwa kipindi hicho wamekuwa wakitenga asilimia moja ya faida yao kama sehemu ya uwajibikaji kama sehemu kwa jamii inayowazunguka.
Akipokea msaada huo ,Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Beno Malisa amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki matukio ya afya toka mwanzo.
Aidha amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kwa kuweka miundo mizuri ya afya na kusema eneo la afya kuna ushahidi ambao unaonyeaha, Benki hiyo ni ya wengi katika kusapoti eneo la afya .
Mbali ya kushukuru amesema,NMB imekuwa wadau wakubwa kwenye eneo la elimu wamejipambanua kwa vitendo zaidi wanaendelea kuwaomba wakiamini kwamba kwenye mgao wao basi maeneo hayo mawili yatapewa kipaumbele.
“Niwashukuru hapa tuna wodi 11,leo tumepata Magodoro 20 na vitanda 20 hivyo niombe wadau wengine kujitokeza kwani uongozi uhitaji mkubwa kwani bado tuna nyingine za wagomjwa.
“Tunashuru Benki ya NMB imetusaidia kupata vitanda kwasababu tulikuwa na upungufu mkubwa wa vitanda hivyo na kushindwa kulaza wagonjwa wetu katika mazingira mazuri sehemu nzuri ,tulikuwa tunashindwa kulaza wagonjwa , tunaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia kwani tunauhitaji wa vifaa vingine.


More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi