Na Bakari Lulela ,Timesmajira
Chama Cha National League For Democracy(NLD) Kikiongozwa na Mgombea Wa Urais, Doyo Hassan Doyo, Kinawasilisha Ilani yake Kama Dira Ya Matumaini Mapya Kwa watanzania.
Akizungumza jijini Dar es salaammgombea huyo amesema kuwa ilani hiyo Inakusudia Kutatua Changamoto mbalimbali Zinazolikabili Taifa Letu Kwa Kutumia Sera Madhubuti, Sheria bora, Na Mifumo Jumuishi Inayozingatia Usawa,Haki, Na Maendeleo Endelevu .
“Ilani hiii imeandaliwa Kwa Kuzingatia Katiba yaJamhuri ya Muungano Wa Tanzania ya mwaka 1977, Malengo ya Maendeleo Endelevu(Sdgs), Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025,na Takwimu rasmi Kutoka Ofisi Ya Taifa ya Takwimu (NBS), Benki ya Dunia (World Bank), Na Mashirika ya Kimataifa Katika Muktadha Wa Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii Unaoendelea Kubadilika Kwa Kasi ndani na nje ya Tanzania, “amesema Doyo
Aidha chama cha NLD Kinatambua Umuhimu Wa Kuwa na Ilani inayojibu Changamoto halisi za Kuweka Msingi wa Mabadiliko ya Kweli ilani hiyo imetungwa Kama nyenzo ya Kuongoza Mwelekeo wa Taifa Katika Miaka Ijayo, ikilenga Maendeleo ya Watu, Ustawi wa Jamii na Matumizi ya rasilimali Kwa ajili ya Vizazi vya Sasa na Vijavyo.
Kwa upande wake Katibu wa ilani Fahad Doyo amesema kuwa NLD inaamini Kuwa Kila mtanzania ana haki ya Kuishi Maisha yenye heshima, Fursa Sawa na Mazingira wezeshi ya Kuchangia Maendeleo ya Taifa.
‘Kwa Msingi huo, Ilani hiyo inalenga naKuhakikiasha Kuwa rasilimali za nchi Sera za Umma na Taasisi Za Serikali zinaelekezwa Katika Kuleta Mabadiliko Chanya kwa wananchi wote bila ubaguzi ilani hiyo imeandaliwa Kwa Kushirikiana na Makundi Mbalimbali ya Kijamii ya Vijana, Wanawake, Wazee, Wakulima, Wavuvi, Wafanyakazi, Madereva, Wafanyabiashara na Watu Wenye Ulemavu Kwa Lengo la Kuunda Dira Ya Pamoja ya Kujenga Tanzania Mpya yenye Matumaini.
‘Kuhifadhi na Kuongeza thamani ya rasilimali za Taifa Kwa vizazi vijavyo,Ujenzi wa Taasisi imara Zenye Kuwajibika Kwa wananchi, Maendeleo yanayozingatia Mazingira na Matumizi endelevu ya teknolojia Malengo ya Kimsingi ya Ilani hiyo’Uzalendo haki na Maendeleo Kuibua Fursa Mpya za Maendeleo ya Watu na Taifa katika Kuwapatia Wananchi huduma bora Za Ki ijamii na Kiuchumi Kuwezesha Ushiriki wa Kila Mtanzania Katika Uchumi Wa Taifa,Kupambana na Umaskini, Ukosefu Wa ajira, na Ukosefu wa Fursa za Kujenga Taifa

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina