December 31, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nkasi wapitisha Rasimu Bajeti ya Bil. 37.7

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Nkasi

HALMASHAURI ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa imepitisha rasimu yake ya bajeti Kwa mwaka 2024-25 ambapo inatarajia kukusanya na kutumia kiasi Cha Shilingi 37,705,501,400:00 kama bajeti kuu Kwa mwaka wa fedha 2024-25 Huku kiasi Cha Shilingi 3,294,826,400:00 kikitarajiwa kutoka kwenye mapato ya ndani.

Akizungumza Kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi afisa mipango na uratibu Steward Vidoga amesema kuwa katika kufanikisha utekelezaji wa bajeti hiyo kunategemea mapato ya ndani,kutoka serikali kuu na kutoka Kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.

Amesema kuwa licha ya kuzingatia vipaumbele mbalimbali vya halmashauri wanatarajia kukusanya na kupitia mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na vyanzo mbalimbali ikiwemo fedha kutoka serikali kuu.

Vidoga ameainisha mchanganuo wa bajeti hiyo kwa upande WA makusanyo ya ndani kuwa ni Matumizi ya kawaida 2,184,049,480.00,Mishahara 71,391,360.00,Miradi ya maendeleo 1,039,385,560.00,Mapato fungwa 695,112,500.00 ambapo jumla ndogo ni 3,294,826,400.00.

Pia halmashauri inatarajia kukusanya jumla ya shilingi 34,410,675,000.00 kutoka serikali kuu na mapato hayo kutumika katika mchanganuo ufuatao ambao ni Matumizi ya kawaida 1,465192,000.00, Mishahara 21,082,510,000.00, Miradi ya maendeleo 11,863,063,000.00 na kuweza kupata jumla kuu ya 37,544,430,000.00.

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya Williamu Mwakalambile Kwa upande wake amedai kuwa katika kipindi hiki Cha mwaka wa fedha WA 2024-25 halmashauri inatarajia kuanzisha shule ya msingi yenye mchepuo wa Kiingereza kama sehemu yake ya mradi katika kama chanzo kingine Cha Mapato katika halmashauri hiyo.

Alidai kuwa mchakato wa Mpango huo umekamilika Kwa maana ya maamuzi katika vikao mbalimbali vya kisheria Kwa maana walikua wamependekeza miradi miwili yaani kuanzisha hotel au shule ya mchepuo wa Kiingereza lakini la uanzishwaji wa shule limeweza kuafikiwa na wote wakiwamo Madiwani