December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Njombe kufanya Kongamano kuliombea Taifa na Samia

Na Yusuph Mussa, TimesMajira Online, Njombe

MKOA wa Njombe umeandaa Kongamano la kuliombea Taifa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuona amani, utulivu na umoja vinaendelea kutamalaki hapa nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba aliyasema hayo Julai 22, 2022 kwenye mkutano wa mwisho wa Kamati ya maandalizi ya kongamano hilo litakalofanyika Julai 29, 2022 kwenye Ukumbi wa Lunyanywi mjini Njombe.

“Wajumbe, hiki ni kikao cha mwisho na maandalizi yanakwenda vizuri. Uamuzi tuliochukua kama mkoa wa kuliombea Taifa na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, ni wa busara, na kuonesha kuwa tunajua umuhimu wa kuliombea Taifa na Rais wetu ili nchi iendelee kuwa na amani, mshikamano na umoja.

“Ni imani yangu makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo viongozi wa Serikali, kisiasa, wataungana na viongozi wa dini, viongozi wa mila na machifu katika kuliombea Taifa” alisema Kindamba.

Kabla ya kongamano hilo, Julai 28, 2022, Kamati hiyo inayoshirikisha viongozi wa dini zote, viongozi wa mila na utamaduni, machifu, wakuu wa wilaya, makatibu tawala, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri, watatembelea miradi ya maendeleo kwenye halmashauri za Mkoa wa Njombe ili kuona kazi zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Miradi hiyo ni pamoja na ile ya afya, elimu, ujenzi wa miundombinu majengo ya Serikali na barabara ambayo utekelezaji wake unafanyika kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri, Serikali Kuu pamoja na wafadhili.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa alisema Njombe wameamua kufanya kongamano hilo la kuiombea nchi na Rais Samia, kama ishara ya kumuunga mkono Rais Samia kwa kazi nzuri anazoendelea kufanya ikiwa ni pamoja na kupeleka fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi.

“Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya kazi kubwa tangu kuingia madarakani. Na amekuwa akizunguka ndani na nje ya nchi kuona wananchi wake wanapata maendeleo. Kwa jitihada hizo za Rais na Serikali yake, tumeona tumuombee Rais pamoja na nchi ili tuendelee kusonga mbele tukiwa na amani na utulivu” alisema Kasongwa.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba (katikati) akiendesha kikao kama Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Julai 29, 2022 mjini Njombe. Wengine ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Wakili Msomi, Hilmar Danda (kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa (kulia). (Picha na Yusuph Mussa).
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Julai 29, 2022 mjini Njombe wakiendelea na kikao. Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe (DED) Sharifa Nabalang’anya (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe (TD) Kuluthum Sadick (kushoto). (Picha na Yusuph Mussa).
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Julai 29, 2022 mjini Njombe wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Julai 29, 2022 mjini Njombe wakiwa kwenye kikao
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Julai 29, 2022 mjini Njombe wakiwa kwenye kikao. (Picha na Yusuph Mussa).
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Julai 29, 2022 mjini Njombe wakiwa kwenye kikao. (Picha na Yusuph Mussa).