Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimewakaribisha vijana kufikia katika Banda lao lililopo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Sabasaba(DIFT) ili wapate elimu ya kina kuhusu kozi ya Urubani.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho hayo Mkufunzi wa Urubani kutoka Chuo hicho, Ashrafa Ramadhan amesema chuo hicho tayari kimeishaanza rasmi kutoa mafunzo ya urubani kwa vitendo kwa vijana wa kitanzania.
“Mafunzo Urubani tayari yameanza kutolewa na wanafunzi wa kwanza 10 wamejiunga, wakiwemo wanawake wanne na wanaume sita tunavyo vifaa vya kisasa na wataalamu waliobobea katika nyanja hiyo”amesema
Ramadhan amesema NIT imejipanga vizuri kuanzia hatua za awali za kumfundisha Mwanafunzi kuanzia ardhini hadi mafunzo ya angani.
Akitaja sifa za kujiunga na mafunzo hayo amesema ni kuanzia elimu ya kidato cha nne, na umri wa kuanzia miaka 17 na kuendelea.
Aidha amesema kuwa NIT imewekeza katika miundombinu na teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mafunzo bora ya kitaalamu na ya kimataifa.

More Stories
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini