Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MUIGIZAJI wa filamu hapa nchini Salma Jabu maarufu kama ‘Nisha’, amewapa makavu wanaume wa Kitanzania kuwa waache tabia ya kuwaongopea wanawake jambo linalochangia mwanamke kufanya maamuzi magumu kwenye mahusiano.
Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram mara baada ya aliyekuwa mpenzi wake kufunga ndo na mwanamke mwengine Nisha amesema, amempongeza mwanaume huyo kwa kua mkweli mara baada ya kumtaalifu anataka kuoa.
“Huyu ni Ex wangu na leo anafunga ndoa na nguo ya harusi ya mkewe mimi ndio nimemuagizia, najisikia furaha sana. Kwanini nimeshare hapa? kwanza kama ‘inspiration’ kwangu na ushuhuda wa mapenzi ya kweli, kwa hiyo eye ni kama kaka yangu na tuko sawa kabisa.
“Huyu mwanaume amekuwa mkweli sana na hata kutengana sababu moja wapo(zipo muhimu) tulitengana sababu tu ya utaifa na sikuweza kuacha maisha yangu Tanzania na kwenda nchi nyingine kuwa mtu mwengine na hata yeye hivyo hivyo.Pamoja na yote amekuwa akinambia kila kitu hadi hili kukamilika hadi nguo kuorder na mengineyo.
“Nimelileta hili kwenu Wanaume wa Kitanzania, mjifunze kama Mwanamke unaona huyu si mke wangu kuna kikwazo hiki na kile mchane na sio kumdanganya, mna msemo wenu Mwanamke bila kudanganywa haendi, acheni hizo fikra potofu, wanawake wote tunaojitambua tunapenda wanaume wakweli, niambie ukweli hata kama utauma vipi, nikipoa nirahisi kukusamehe kuliko ukinidanganya.
“Naomba niwasemee wasanii wa kike wa Tanzania wanaodate na waliowazidi umri au kipato?. Wengi wamekuwa wahanga wa kutendwa na walio sawa nao na ndio maana wanaona bora niwe na mtu nnayeweza kumcontrol hata nikiachana Naye siumii kivile sababu nitapata tu kama yeye. Ila uongo wenu wanaume ndio unasababisha wanawake wengi wanakuwa na dharau. Tunawapenda wanaume zetu wa Kitanzania il punguzeni uongo na uhuni,” amesema Nisha.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio