Judith Ferdinand,Mwanza
Wito umetolewa kwa waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kujiunga na bima mbalimbali ikiwemo bima ya ajali binafsi (personal accident), ili kunufaika na huduma ya bima hiyo inayotolewa na Shirika la Bima(NIC).
Hayo yameelezwa na Meneja wa NIC Kanda ya Ziwa Stella Marwa,wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea ofisini kwake kwa ajili ya kueleza mipango na shughuli za shirika hilo ikiwa ni wiki ya wadau wa habari kutembelea na waandishi wa habari ambao ni wananchama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza(MPC).
Ambapo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika hafla ya usiku wa wadau wa habari Kanda ya Ziwa na waandishi wa habari iliondaliwa na MPC kwa udhamini wa wadau mbalimbali itakayofanyika Octoba 20,2023 jijini Mwanza.
Stella ameeleza kuwa bima ya ajali itawanufaisha waandishi wa habari kutokana na ukweli wa mazingira ambayo wanamfanyia kazi mfano wakati anatimiza majukumu yake mtu ajafurahishwa na kazi yake ambayo ameiandika ikatokea akapigwa na kupata majeraha bima hiyo itamsaidia gharama zote za matibabu.
“Itakulinda wewe ukiwa kazini au nje ya kazi endapo utapata ajali au madhira kazini ya kupigwa na kujeruhiwa, hivyo wakati ni sasa wa kujiunga na hii bima ya personal accident ili iweze kuwakinga na majanga ambayo yanaweza kujitokeza mkiwa katika shughuli zenu za uandishi wa habari,”ameeleza Stella.
Mbali na bima ya ajali pia shirika hilo linatoa bima ya maisha,bima ya vyombo vya moto,bima za nyumba,bima za mifugo,bima za wakandarasi pamoja na bima zingine.
Ambapo amewahimiza wananchi kukakata bima ya vyombo vya moto ili kupunguza madhara yanayotokea kwenye jamii huku akitolea mfano Mkoa wa Mwanza hivi karibuni kuna ajali ikitokea ya wakimbia kwa miguu kupata ajali ya kugongwa na gari na kwa bahati mbaya wale watu hawakuwa na hata na bima ya personal accident ambayo ingewasaidia warithi wao kupata kifuta machozi na waliopata majeraha wangeweza kutibiwa kwa ile bima huku mmmiliki wa chombo angekuwa amekata bima ya chombo cha moto gari yake ingeweza kutengenezewa.
“Kwa upande wa bima za vyombo vya moto tuna pikipiki,bajaji,magari ambapo kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani lazima mtumiaji yoyote wa chombo cha moto awe na bima ata kama ni ndogo ambayo inaweza kumsaidia yeye mwenyewe pamoja na watembea kwa miguu,”.
Bima ya nyumba pia inawasaidia wananchi sana kwani inamlinda pale anapopatwa na majanga yasiyozuilika kama mafuriko au moto hivyo ametoa wito kwa wananchi kukata bima hiyo ili endapo yakitokea majanga wasianze kulalamikia serikali au kusubili msaada bali bima hiyo itawasaidia kurejesha tababsamu.
Wote tunasikia kupitia vyombo vya habari kuwa kuna mvua kubwa zitanyesha hapa nchini sasa niwashauri wananchi mkate bima ya nyumba hii italinda nyumba na majanga,msipuuze wataalamu wa utabiri wa hali ya hewa maana wamesema kuna hizo mvua kubwa na zinaweza kuleta madhara sisi NIC tupo tayari kuwalipa fidia kupitia bima ya nyumba,”amesema Stella.
Ameeleza kuwa NIC imetimiza miaka 60 Oktoba 16,2023 lakini wamekuwa wakishirikiana na waandishi wa habari kuhakikisha wanafikisha elimu ya bima kwa wananchi.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa