January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NIC yawalipa makampuni 11 yaliyonunua mazao ya korosho Mkoani Lindi na Mtwara

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Shirika la Bima la Taifa (NIC) limelipa shilingi milioni 46 Makampuni 11 ambayo hununua mazao ya korosho Mkoani Lindi na Mtwara na ambayo yamekata Bima kutoka NIC kutokana na uharibifu wa mazao hayo.

Akizungumza na waandishi wa mara baada ya kukabidhi hundi kwa wafanyabiashara wa Korosho Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Yesaya Mwakifulefule amesema malipo ya Bima hizo ni kutokana na hasara iliyotokana na unyaufu wa mzigo koroshokuwa uliokua umehifadhiwa ktk maghala mbali mbali mikoani humo.

Mwakifulefule amesema kuwa NIC iko katika kuhakikisha wafanyabiashara na wakulima kupitia Bima ya Kilimo wanakuwa na na amani na uhakika wa mitaji yao pindi wanapofikwa na majanga na kufanya biashara iendelee kutokana na bima walizozikata kutoka NIC.

“Sisi ndiyo Bima tupo kwa ajili kutoa huduma bora kwa wateja pamoja na kufanya biashara kuwa endelevu na mitaji ikiwa salama kuendeleza kuwekeza maradufu katika sekta ya kilimo”amesema Mwakifulefule.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani Sangye Bangu amesema kuwa taasisi zingine ziige kwa bima ya NIC pamoja na kutoa huduma.

Amesema kuwa wafanyabiashara katika sekta ya korosho wananeemeka na NIC kwa kwa kurudishiwa hasara waliopata uchakavu.