January 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

‘Ni Wasira ‘Makamu Mwenyekiti CCM Bara

Na Agnes Alcardo na Joyce Kasiki,Dodoma

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtangaza, mwanasiasa mkongwe nchini, Stephen Wasira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Wasira amepita kwa kishindo ambapo amekosa kura kumi na Moja tu kati ya kura zote zilizopigwa .

Dkt. Samia alimtangaza Mzee Wasira baada ya kushinda kwa kura 1,910 kati ya kura 1,921 kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye Mkutano Mkuu wa CCM mwaka huu jijini Dodoma, ambapo ushindi huo ni sawa na asilimia 99.42

Kati ya kura zilizopigwa na wajumbe hao, Kura halali ni 1,917, zilizoharibika ni nne hulu Kura za hapana zikiwa Saba.

Aidha kwa upande wake, Makamu mwenyekiti huyo mpya Stephen Wasira, amesema kuwa CCM ni chama cha amani hivyo yajivunia kuendelea kuwa katika chama hicho na kupata nafasi hiyo.

Amesema, anashukuru sana kwa nafasi hiyo analiyopewa na atahakikisha anashirikiana vizuri na viongozi wengine.

Nao baadhi wajumbe wamemzungumzia wasira kwamba ni mtu sahihi atakayekivusha CCM salama kwenye Uchaguzi Mkuu ujao .

Amesema jina la Wasira ni bingwa wa kujenga na kubomoa hoja huku akisema ni mtu sahihi kwa mazingira sahihi na mahitaji sahihi.

Naye Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara amesema lichabyabumri wake kuwa mkubwa lakini akili yake ipo timamu.

Amesema katika mwaka huu wa Uchaguzi Chama kimepata mtu wa kujenga hoja na kumsaidia Mwenyekiti kujenga chama