Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
SHIRIKA la nyumba la Taifa (NHC) limetoa msaada wa vyakula mbalimabli kwa msikiti wa Al Madina uliyopo Msakuzi, Mbezi Mkoani Dar es Salaam kwaajili ya iftar kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwenye kipindi hiki wakiwa katika funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 21, 2024 Mbezi Mkoani Dar es Salaam Afisa Uhisiano wa Shirika la Nyumba la Taifa Yamlihery Ndullah amesema jukumu la kutoa msaada kwa watoto hao ni jukumu la jamii nzima kwani katika watoto hao watapatikana viongozi wa dini na Taifa hapo badae.
Aidha, Afisa Uhisiano wa Shirika la Nyumba la Taifa Yamlihery Ndullah amesema jambo hilo ni muendelezo wa shirika la Nyumba la Taifa katika kuendelea kutoa misaada kwenye sehemu mbalimbali zenye mahitaji, pia kupitia kwa Mkurugenzi wa NHC Hamad Abdalah, wataendelea kutoa misaada hiyo ili kuendelea kupeleka faraja na furaha kwa watu wote Nchini.
Kwa upande wake, Imamu wa Msikiti wa Al Madina Sheikh Jumaa Salum Mhando amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa msaada huo mkubwa ambao utawasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kuweza kufuturu na kufunga funga zao vyema katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
“lengo ni kuwawezesha na kuwakamua katika hali ya kimaisha kwa kuwa wanaishi kwenye mazingira magumu, hivyo tunawapongeza NHC kwa kuleta neema hii katika mwezi maalumu kwa sababu mwezi huu ni mwezi wa kuchuma heri nyingi, waliofanya hivi Mungu atawazidishia zaidi ya hapa na Mungu atawajalia wepesi katika shughuli zao” amesema Sungura
Hivyp, Imamu wa Msikiti wa Al Madina Sheikh Jumaa Salum Mhando ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau mbalimbali kuwasaidia katika kutoa sadaka ambazo zitawasaidia kuwakwamua watoto ambao wanapitia wakati mgumu, pia kuwasaidia katika kumalizia jengo hilo la msikiti ambalo bado halijakamilika
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba