January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ng’ong’a:siwazi kugombea Ubunge mwaka 2025

Na Suleiman Abeid,Timesmajira Online, Shinyanga

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Gerald Ng’ong’a, ameeleza kuwa  kwa sasa awazi  suala la kutaka kugombea Ubunge  mwaka 2025  katika Jimbo la Rorya kwani  siyo kipaumbele chake.

Ambapo kipaumbele chake ni  kuhakikisha anapeleka maendeleo kwa wananchi wa Rorya katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara huku 

Ng’ong’a ametoa kauli hiyo katika hafla fupi ambayo imeandaliwa kwa ajili ya  kuwakutanisha watu mbalimbali ambao ni wazawa wa Wilaya ya Rorya wanaoishi mkoani Shinyanga  ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka,iliofanyika mkoani Shinyanga.

Ambapo amesema watu wengi wamekuwa wakimshauri na kumuomba kwamba mwaka 2025 ajipange kwa ajili ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Rorya hivyo amesikia sauti za watu zao lakini  kwa sasa bado hajafika uamuzi huo huku akisisitiza kuwa  kazi hizo ni ngumu zinahitaji ujasiri

“Ninapokea mawazo yenu mazuri ya kunitaka nipande juu, lakini naomba niwaambie kuwa jambo hili ni zito, eleweni maendeleo ni hatua kwa hatua, wakati wa mimi kusonga pale ninyi mnapotaka nipite, basi Mungu atatuongoza hatujui ni lini, inaweza kuwa 2025 au isiwe 2025, lakini dhamira yangu ni kuwatumikia wana Rorya,”amesema Ng’ong’a.

Pia amesema kuwa  kupitia nafasi yake ya Uenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya anataka kuhakikisha changamoto nyingi zilizokuwa zikiikabili halmashauri hiyo miaka ya nyuma zinapungua kwa kiasi kikubwa kama siyo kumalizika kabisa.

“Kwa sasa nimejikita zaidi kwenye nafasi yangu  ya Ueyekiti wa Halmashauri ya Wilaya kwa kuwatumikia wananchi,nimekuwa  nikitembelea kila Kata kuhimiza maendeleo,siko tayari kukubali kuhongwa na yeyote, na moja ya mambo ninayochukia ni mtu kujaribu kunihonga, kipaumbele ni kuwaletea maendeleo,”amesema Ng’ong’a.

Amefafanua kuwa pamoja na kupigania maendeleo ya Rorya lakini pia amekuwa akisimamia kikamilifu fedha za halmashauri kwa kuhakikisha kila fedha inayopatikana inatumika kwa lengo lililokusudiwa na siyo kuhujumiwa na mpaka hivi sasa wapo watendaji wawili amewaachishwa kazi kwa kosa la matumizi mabaya ya fedha za halmashauri.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Gerald Ng’ong’a, akizungumza katika hafla fupi ambayo imeandaliwa kwa ajili ya  kuwakutanisha watu mbalimbali ambao ni wazawa wa Wilaya ya Rorya wanaoishi mkoani Shinyanga  ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka,iliofanyika mkoani Shinyanga.

Baadhi ya wazawa wa Halmashauri ya Rorya wanaoishi mkoani Shinyanga wakimsikiliza mwenyekiti wa Halmashauri yao kwenye hafla fupi ya Sikukuu ya Pasaka.