December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ngombale: Mkinichagua waliobomolewa watalipwa fidia

Na Rose Itono, TimesMajira Online, Dar es Salaam

MGOMBEA Ubunge katika Jimbo la Kibamba mkoani Dar es Salaam kupitia Chama Sauti ya Umma (SAU), Kunje Ngombale Mwiru amesema endapoa atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha wanancho wote wa jimbo waliovunjiwa nyumba kupisha ujenzi wa barabara watalipwa fidia.

Akizungumza katika ziara ya kuwasalimia wananchi wa jimbo hilo, Ngombale amesema licha ya wananchi kulipwa kifuta jasho pia atawaletea maendeleo wakazi hao.

“Endapo mtanipa ridhaa ya kuwa Mbunge nitahakikisha ninawaletea maendelo ya uhakika ikiwa ni pamona kujenga kiwanda ambacho kitatoa ajira kwa vijana wa Jimbo la Kibamba,” amesema Ngombale.

Akiwa katika ziara hiyo amesema, sera ya chama chake ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya afya bila malipo ikiwemo elimu hadi chuo kikuu bure.

Amesema, sera ya SAU katika uchaguzi wa mwaka huu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu ni afya bure, maji bure, elimu bure kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu.

“Mimi ni mtekelezaji wa vitendo naomba mnichague ili niwaletee maendeleo ya uhakikia, nitahakikisha kiwanda kinajengwa katika jimbo hilo ili vijana waweze kuja mapesa mifukoni, hayo malengo SAU,” amesema.

Amesema, SAU ina uhakika wa kupata ushindi wa kishondo katika jimbo hilo kwani hata vyama vingine vya upinzani vinamkubali kutokana dira ya mgombea huyo.