Na Mwandishi Wetu
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekubali rufaa 24 na kuwarejesha wagombea udiwani katika orodha ya wagombea udiwani.
Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Mlangarini (Arumeru Magharibi), Nduruma (Arumeru Magharibi), Nkungulu (Magu), lbungilo (flamela), Itumbili (Magu), Mlandege (Iringa Mjini), Mdoe landeni Mjini), Sinza (Ubungo), Kisongo (Arumeru Magharibi) Uhuru (Dodoma Mjini), Bunju (Kawe), Kwa Kilosa (Iringa Mjini) na Kimbiji (Kigamboni).
Nyingine ni Msambweni (Tanga Mjini), Nsalala (Mbeya Vippni), Nzuguni (Dodoma Mjini), Madukani (Dodoma Mjini), Kerege (Bagamoyo), Kibaoni (Kilombero), Kolo (Kondoa Mjini), Lumemo (Kilombero), Melela (Mvomero) na rufaa mbili za Kata ya Moivo (Arumeru Magharibi).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume wa NEC, ilieleza kwamba rufaa 19 za wagombea udiwani ambao hawakuteuliwa zimekataliwa.
Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Duru (Babati Vzppni), Nundu (Nyang’hwale), Magugu (Babati Vijijini), Sangamwalugesha (Maswa Mashariki), Pongwe (Tanga Mjini), Mpandangindo (Peramiho), Mji Mwema (Kigamboni), Kinampanda (Iramba Magharibi), Mbelekese (Iramba Magharibi), Maendeleo (Mbeya Vijijni), Nalasi Mashariki (Tunduru Kusini), Nyakabindi (Bariadi), Nzovwe (Mbeya Mjini), Ndulungu (Iramba Magharibi)
Kata zingine ni Kwediyamba (1-landeni Mjini), Kyengege (Iramba Magharibi), Kisiriri (Iramba Magharibi), Maluga (Iramba Magharibi) na Ndago (Iramba Magharibi)
Aidha NEC imekataa rufaa 6 za kupinga wagombea udiwani walioteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Kisanga (Kalambo), Mwigobero (Musoma Mjini), Kirima (Moshi Vippni), Gangilonga (Iringa Mjini), Majengo (Mbeya Mjini) na Lipangalala (Kilombero). Idadi hiyo inafanya jumla ya rufaa za wagombea udiwani zilizotolewa uamuzi kufikia 244.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango