Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
KWA mara ya kwanza Wachezaji jijini Dodoma wapata fursa baada ya Mashindano ya Ndondo Cup kufanyika kwa miaka 9 mfululizo Jijini Dar es salaam sasa zamu ya mashabiki wa Soka Mkoani Dodoma kuyashuhudia michuano hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo,Mratibu wa Mashindano hayo,Yahaya Mohammed ‘Mkazuzu’ amesema jumla ya timu 16 zinatarajia kushiriki mashindano hayo.
Amesema kwa Mkoa wa Dodoma bingwa anatarajia kuondoka na kitita cha Shilingi milioni 5 huku mshindi wa pili akijipatia Shilingi milioni 3 na kikundi bora cha ushangiliaji kikilamba Shmilioni moja
“Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma ndio watasimamia kila kitu na ada itakuwa Sh200,000 kauli mbiu yetu ni twende pamoja hivyo ni lazima twende pamoja na vijana wa Dodoma,”amesema Mkazuzu
Uzinduzi huo ulishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kilimo,Antony Mavunde ambapo amewapongeza waandaaji wa mashindano hayo kwa kuleta fursa kwa vijana wa Dodoma kwani hiyo itakuwa ni fursa kwa baadhi ya timu kupata wachezaji kupitia mashindano hayo.
“Dodoma hatupendi kushindwa tumejipanga kwa hii fursa na naamini tutawashinda watu wa Dar es salaam,tunataka yawe mashindano endelevu kwa ajili ya timu zetu Dodoma Jiji na Fountain Gate kuvuna wachezaji,”amesema.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) Majuto Msekela amesema wapo tayari kuandaa mashindano hayo kwa kuweka waamuzi ambao watatafsiri sheria vizuri pamoja na kutafuta viwanja ambavyo ni rafiki kwa kucheza.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025