Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saud Al-Shidhani yaliyolenga kuimarisha na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya nishati. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, tarehe 17 Februari 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, wamejadili kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu wa kitaalamu, mafunzo kwa wataalamu, teknolojia ya uchimbaji pamoja na usimamizi wa miradi ya gesi na mafuta kwa lengo la kuharakisha maendeleo kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Shirika la Maendeleo ya Mafuta la Oman (PDO).




More Stories
Wizara,TPSF kuongeza ushiriki kongamano la kiswahili
Prof.Mbawara:TMA yakamilisha ufungaji wa mitambo miwili ya uangazi wa hali ya hewaÂ
PBPA yapongezwa kwa usimamizi wa upatikanaji wa Mafuta nchini