Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Morogoro
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema,endapo chama hicho kitashika dola tena,Serikali yake itaandaa mkakati wa kutumia ndege nyuki “Drones” kufukuza wanyama waharibifu wa mazao kama tembo.
Balozi Dkt. Nchimbi amesema hayo Oktoba 18, 2025 kwenye mkutano wa kampeni, uliofanyika katika Kata ya Mwaya, Kilombero mkoani Morogoro, ikiwa ni muendelezo wa kampeni za CCM,na huo kuwa Mkoani 25 kufikiwa na kiongozi huyo.
Amesema, lengo la matumizi ya ‘drone’ ni kuhakikisha wakulima wanaondokana na tatizo la kuharibiwa kwa mazao yao ambayo uchangiwa na wanyama.
“Tutashirikiana kuhakikisha mipango ya Serikali ya kutumia ndege aina ya drone kuwafukuza wanyama waharibifu inakwenda kufanyika ili mazao ya wakulima wetu yabaki salama na nchi yetu iendelee kupata maendeleo,” amesema Dkt. Nchimbi

More Stories
Wizara,TPSF kuongeza ushiriki kongamano la kiswahili
Prof.Mbawara:TMA yakamilisha ufungaji wa mitambo miwili ya uangazi wa hali ya hewaÂ
PBPA yapongezwa kwa usimamizi wa upatikanaji wa Mafuta nchini