Na Rose Itono,TimesMajira Online.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefungua Kongamano Maalumu la Maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kuitaka jamii, kuyaishi na kuyaenzi matendo ya Nyerere wakati wa uhai wake.
Pia amezitaka taasisi za elimu kufanya tathmini za mitaala, ili kuona kama inakidhi matakwa ya sasa kwa maendeleo ya nchi sambamba na kuchukua maoni kwa wadau mbalimbali lengo likiwa ni kuboresha.
Akizungumza kwenye kongamano hilo lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam, amesema mada kuu ya kongamano ni Falsafa ya Mwalimu Nyerere katika elimu na uchumi kwa ajili ya maendeleo endelevu.
“Mapitio ya mitaala, kufanya tathmin na kuchukua maoni mbalimbali kutoka kwa wadau, yatasaidia kuboresha sekta ya elimu,” amesema.
Amesisitiza kuhakikisha mitaala itakayofaa, itawezesha wanafunzi kuweza kujitegemea kwa kuwa na michepuo itakayowawezesha wanafunzi, kujifunza kwa nadharia na vitendo.
Amsema Wizara, iko tayari kuongeza fursa kwenye shule za michepuo huku akisisitiza kazi za mikono mashuleni zisipuuzwe.
Naye mmoja wa watoa mada kwenye kongamano hilo, Ludovick Utoh aliyewahi kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema mitaala ya elimu, iendane na hali ya sasa kwa kuhakikisha kunakuwa na mfumo utakaomuwezesha mwanafunzi kujiajiri.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam