Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameeleza kuwa, nia ya chama hicho ni kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), chini ya Mwenyekiti wake Deodatus Balile, uliofanyika Aprili 4, 2025 mkoani Ruvuma,amesema, dhamira ya kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari imeendelea kuonekana, hususani katika kipindi hiki cha Dkt.Samia Suluhu Hassan.

“Kwa niaba ya CCM na watanzania wote wapenda amani, tunawashukuru sana Wahariri na kwa kupitia kwenu Waandishi wa habari, kwani katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wenu Balile imeonesha wazi jinsi uhuru wa vyombo vya habari ulivyo imarika hususani katika kipindi hiki chini uongozi wa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Na kweli kwani hata katika taarifa ya Baraza la Habari ya mwaka 2022/2023 inayoongelea The State of Media In Tanzania, inasema kwa kina kuwa kuna mabadiliko makubwa ya uhuru wa habari na uhuru wa kutoa maoni katika nchi yetu na umeimarika.Lakini hata katika taarifa ya kimataifa kuhusu uhuru wa vyombo vya habari pia, nchi yetu imeonekana kupanda kwa zaidi ya nafasi 50 katika vipindi vya miaka mitatu kwa maana nyingine tumezipiga nchi nyingine 50 katika kipindi cha miaka hiyo,” amesema Balozi Nchimbi.

More Stories
Polisi Mbeya yajivunia miaka minne ya mafanikio
Wahariri wa vyombo vya habari nchini wapongezwa
Balozi Nchimbi: Uchaguzi upo palepale hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia