October 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nchimbi asimamishwa Hedaru, asisitiza umoja wa kimataifa

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Tanga
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo Juni 7, 2024 akiwa njiani kuelekea Tanga, baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoa wa Kilimanjaro kwa kufanya mkutano wa ndani Wilaya ya Same, umesimamishwa na wananchi katika eneo la Hedaru, wakitaka awasalimie.

Akiwa Hedaru Dkt. Nchimbi ameendelea kuwasisitiza Watanzania kuhusu umuhimu wa umoja wa kitaifa kwa kutunza tunu ya amani iliyopo nchini.

Katibu Mkuu wa CCM na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, anaendelea na ziara ya mikoa mitano inayolenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025,kuhamasisha uhai wa chama hicho kuanzia ngazi ya shina pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majawabu.

Ambapo leo akiwa mkoani Tanga, ameambatana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano Kimataifa (Suki), Rabia Hamid Abdallah.