Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MICHUANO ya mchezo wa Cricket ya kufuzu Kombe la Dunia la T20 kwa Wanaume, ICC Kanda A ya Afrika, inaendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Gymkhana na Chuo Kikuu, Dar.
Mashindano hayo yanayozishirikisha nchi 6, yalizinduliwa rasmi Septemba 21 mwaka huu, huku mgeni wa heshima akiwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Neema Msitha.
Aidha, mashindano hayo yanashindaniwa na mataifa sita, ikiwemo Ghana, Cameroon, Malawi Lethoto, Mali na Tanzania ambapo ndio wenyeji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Afisa Habari na mratibu wa mashindano hayo, Atif Salim alisema
michuano hiyo itoa fursa ya Tanzania kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ya T20, iwapo itafuzu kati ya timu mbili za juu.
Salim alisema, michuano hiyo itatoa timu mbili ziweze kusonga mbele ili kufuzu Kombe la dunia la T20 ambayo yatafanyika nchini Sri Lanka na India mwaka 2026.
Alisema, Timu mbili kutoka hapa na timu mbili zingne zitaungana na timu ya Uganda na Namibia, ili ziweze kushiriki michuano hiyo ya Kombe la dunia kwa mchezo wa Cricket.
“Ni safari ndefu ambayo tunaanzia nyumbani na tuna matumaini kwa sababu tupo nyumbani, naamini tutafanya vizuri ili tuwepo kwenye nafasi mbili lakini tunahitaja kuibuka wa kwanza kutokana na ubora wa timu yetu,” alisema Salim.
Hata hivyo alisema, anawaomba Watanzania kuipa sapoti timu ya Taifa ya Tanzania mchezo wa Cricket kwa wanaume iweze kufanya vyema michuano hiyo.
Akizungumzia maandaliz, Salim alisema yapo vizuri kwa kikosi kimeandaliwa kwa ajili ya kuleta matokeo chanya ili kuitangaza nchi yetu.
Alimshukuru Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na atibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Neema Msitha kwa kuwa nao bega kwa bega kuhakikisha mchezo huo unakuwa na vijana wanafanya vyema.
More Stories
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya