December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NBS yatoa mafunzo kwa waandishi wa Habari wa mitandao ya kijamii, maandalizi ya Sensa ya watu na Makazi

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS imeandaa mafunzo kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) lengo likiwa ni kuwajengea uwelewa wanahabari hao kuhusu maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Mafunzo hayo yameanza leo Juni 14, 2022 Mkoani Iringa na yatahitimishwa hapo kesho Juni 15.

Waandishi wa habari kutoka Mitandao Mbali mblai ya kijamii Wakiwa katika Mafunzo Maalum ya Umuhimu wa Sensa ya watu na Makazi, Mafunzo hayo amabyo yameratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Kwa kushirikiana na Jumuiya Mitandaoni ya kijamii Tanzania (JUMIKITA)
Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Said Amir akitoa Mafunzo Kwa Waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii mkoani Iringa kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Mwanasheria Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mary Senapee akitoa Mafunzo Kwa Waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) mkoani Iringa kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Mtaalamu wa Idadi ya watu ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hellen Siriwa akitoa Mafunzo Kwa Waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) mkoani Iringa kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.