Na.Mwandishi Wetu,TimesMajira
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetunukiwa tuzo ya Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha za mwaka 2025 katika kundi la Benki Kubwa, ikiwa ni sehemu ya kutambua ubora, weledi na uzingatiaji wa viwango vya kimataifa katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha.
Tuzo hiyo ilipokelewa na Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Rayson Foya, kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha anayeshughulikia Huduma za Hazina, Nsubili Akomeligwe Kajela, katika hafla ya utoaji wa tuzo zilizoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), iliyofanyika Novemba 26, 2026, katika Ukumbi wa APC, Bunju, jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo inaitambua NBC miongoni mwa benki tano kubwa nchini zilizofanya vizuri katika kuandaa na kuwasilisha taarifa za fedha za mwaka 2025 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uhasibu vinavyotumika katika sekta ya benki.

Akizungumzia mafanikio hayo, Foya amesema tuzo hiyo ni uthibitisho wa juhudi na weledi unaooneshwa na benki hiyo katika kuhakikisha taarifa zake za fedha zinaandaliwa kwa kuzingatia misingi ya uwazi, usahihi na viwango vya kimataifa vya uandaaji wa taarifa za fedha (International Financial Reporting Standards – IFRS).
Ametumia pia fursa hiyo kuishukuru timu nzima ya NBC, ikiwemo uongozi, menejimenti na wafanyakazi wote, kwa mchango wao katika kufanikisha mafanikio hayo.


More Stories
Rais apongeza hatua makubaliano kupunguza vifo mama,mtoto
Bilioni 100 kujenga wodi mama,mtoto Tanzania
EWURA watoa elimu udhibiti huduma nishati na maji