Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Dennis Londo (Mb) ametembelea Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Veronica Nduva Ofisini kwake jijini Arusha.
Katika mazungumzo yao, Londo alimuhakikishia Nduva ushirikiano na kumuelezea kuwa Tanzania itashiriki katika masuala yote yanayohusu Jumuiya ya EAC kwa uzito unaostahiki.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujitambulisha na kufahamiana baada ya Londo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika mwezi Julai 2024.
Londo aliongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM