Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi leo Aprili 14, 2022 amefungua kikao cha wadau kilichoandaliwa na Shirika la USAID kwa ajili ya kujadili matokeo ya utafiti uliofanyika kuhusu athari za UVIKO – 19 katika shughuli za kiuchumi za vijana. Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya mtandao ambao ulishirikisha wadau mbalimbali zikiwemo Wizara zinazo husika na masuala ya vijana Tanzania bara na Visiwani, Wizara ya Kilimo, Viongozi wa serikali kutoka Mkoa wa Iringa na Mbeya pamoja na Shirika la Feed the Future Tanzania.
Naibu Waziri Katambi katika Mkutano huo alielezea mikakati ambayo Tanzania imejiwekea katika kuendelea kutoa fursa mbalimbali kwa vijana zitakazo wawezesha kujikwamua kiuchumi. Pamoja na hayo alipongeza juhudi zilizofanyika kupitia mradi “Advancing Youth” ambao umewanufaisha vijana 38,500 na kusaidia kuzalisha ajira 3,650 kwa vijana katika sekta rasmi na isiyo rasmi.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutambua mchango wa unaofanywa na wadau mbalimbali katika kukuza ustawi na maendeleo ya vijana nchini.
Aidha, maandiko ya matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa na wataalam mbalimbali walioshiriki katika mkutao huo. Pia vijana walionufaika na mradi wa Inua Vijana “Advancing Youth” waliweza kutoa shuhuda kuhusu manufaa ya mradi huo.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi