Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya
MBUNGE wa Viti Maalum, Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ametekeleza ahadi yake ya kutoa magodoro katika gereza la Raunda lililoko jijini Mbeya kwaajili ya mahabusu na wafungwa wanawake.
Mhandisi Mahundi alitoa ahadi hiyo jana alipotembelea sehemu ya Gereza la Wanawake la Ruanda na kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wanawake hao pamoja na kuhaidi kutoa Magodoro (10).
Ombi hilo la magodoro kwa wafungwa na mahabusu lilitolewa juzi na uongozi wa gereza ambapo pia kuna ufinyu wa mabweni ya kulala na huduma za kijamii ambazo mahabusu hao hujitegemea kwa kuuza bidhaa mbalimbali wanazotengeneza kwa mikono zimekuwa msaada mkubwa kwao.
Akishukuru baada ya kupokea msaada wa magodoro kumi, Mkuu wa Gereza la Mahabusu Wanawake, Mrakibu Mwandamizi wa Magareza Rehema Mwailunga amewataka wadau wengine kujitolea kwa moyo kusaidia mahitaji ya mahabusu na wafungwa wa gereza hilo.
“Tunaomba wadau wengine wenye moyo kujitokeza kusaidia kwani mahitaji bado ni mengi, tunafurahi kuona watu wanavyojitokeza, tunamshukuru sana Naibu Waziri wa Maji kwa msaada wa magodoro na mahitaji mengine aliyotoa tunasema asante “ amesema Mwailunga.
Gereza la Mahabusu Ruanda lililoko jijini Mbeya lina mahabusu na wafungwa wanawake 38 na mtoto mmoja.
Naye Naibu Meya wa Jiji la Mbeya, Agness Mangasila amesema kuwa Madiwani Viti Maalum Mkoa wa Mbeya wataendelea kutembelea mara kwa mara ili kuwapa moyo wanawake na kuwapatia mahitaji maalum.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea