Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, llala
Mbunge wa Jimbo la Ilala Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu ,amewataka wadau wa samaki kuacha kujiushisha na uvuvi haramu katika ufukwe wa Bahari ya Hindi kwani unasababisha uharibifu wa mazubgira .
Naibu Spika Zungu alitoa agizo hilo katika sherehe za kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutimiza miaka miwili katika uongozi wake akiwa madarakani .
“Kwa niaba ya Serikali agizo Wadau wa samaki wote waache kujihusisha na uvuvi haramu katika fukwe ya Bahari ya Hindi inasababisha uharibifu wa mazingira “alisema Zungu .
Mbunge Zungu ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Bodi ya soko la Kimataifa la Samaki feri kwa kuandaa siku hiyo Maalum ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake kutimiza miaka miwili ambapo aliwataka kushirikiana na serikali na kukusanya mapato ya soko vizuri.
Mbunge Zungu alisem a Rais Samia ameleta hamasa kubwa Tanzania kwa kuleta usawa katika Demokrasia na vyama vya upinzani ,pamoja na hamasa sekta ya michezo timu zetu za Tanzania zinaendelea Kufanya vizuri mashindano ya Kimataifa yanaitangaza nchi .
Aliitaka Bodi ya soko na Uongozi wa soko la Kimataifa la Samaki feri usimamizi mzuri wa soko hilo
Ili mapato yaweze kuongezeka .
Meya wa halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto alisema Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika nchi yetu Katika Ziara yake Wilaya ya Ilala Maelekezo aliyotoa yote yametekelezwa kwa wakati ikiwemo kufunga solar na maktaba Katika Shule .
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ilala Said Sidde, alisema kwa niaba ya ccm Ilala wanaipongeza chama cha MÃ pinduzi Kivukoni pamoja na Halmashauri ya Jiji kwa Maendeleo mazuri ya soko la samaki feri pamoja na kuandaa Siku Maalum ya kumpongeza Rais kutimiza miaka miwili .
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Saidi Sidde alisema mwaka 2025 Katika Uchaguzi Mkuu Mgombea wa Urais wao Wana Ilala ni Dkt Samia Suluhu Hassan,Rais pekee ameweza kukuza uchumi na kutekeleza Ilani kwa vitendo Wilaya ya Ilala ambapo imeweza kupata miradi mikubwa ya Maendeleo ,Sekta Afya,Elimu ,Barabara ,na Elimu .
Meneja wa Soko la Kimataifa la samaki Feri Dennis Mrema alisema mafanikio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yanaonekana katika Kila Sekta ya Huduma za Jamii ,uchumi ,Miundombinu,Elimu ,kilimo ,uvuvi na Siasa .
Akizungumzia mafanikio ya Soko la feri alisema katika miaka miwili ya Uongozi wake mafanikio makubwa yameonekana mabadiliko Kwa wageni na watalii wengi wa ndani na nje kutembelea Soko hilo.
” Katika miaka miwili ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mafanikio mengine sera ya uchumi wa Bluu imeongeza fursa ya kuongeza raslimali za bahari na makampuni ya nje yameongeza mnyororo wa thamani Kwa mazao ya Bahari “alisema Mrema .
More Stories
Chatanda aridhishwa mwitikio watu kujitokeza kupiga kura Korogwe TC
Wanandoa wawili wamuua mtoto wao,kwa kosa la kujisaidia kwenye nguo
Dkt.Tulia kifo cha Ndugulile kimeacha simanzi kwa Bunge