Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali amefanya ziara ya kushtukiza ya kukagua eneo la kupakua Mafuta kutoka kwenye Meli kuingia bandarini katika kina kirefu cha Bahari eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam.
Mahimbali amefanya ziara hiyo, Machi 29, 2022 kwa lengo la kujionea shughuli zinavyofanyika katika eneo hilo pamoja na mazingira ya kufanyia kazi.
Akiwa katika ziara hiyo alikutana na baadhi ya wafanyakazi katika eneo hilo na kuwaeleza kuwa serikali ya inaendelea kuimarisha na kuboresha sekta ya mafuta nchini ili iweze kuleta tija zaidi kwa taifa na wananchi wake.
Aidha aliwasisitiza wafanyakazi hao kufanya kazi kwa weledi wakizingatia maslahi mapana na nchini yetu.
Picha mbalimbali zikionyesha ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (mwenye miwani) katika eneo la upakuaji mafuta katika kinakirefu cha bandari Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua