Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Nairath Ramadhani maarufu kama ‘​Official Nai amempa makavu dada mmoja ambaye jina lake hakuliweka hadharani kuwa aache mara moja kumfuatilia na badala yake amemtaka kujifunza jinsi ya kumtunza mwanaume wake.
Akitoa makavu hayo kupitia kwenye Ukuarasa wake wa Instagram Nai amesema, alinyamaza kwa mda mrefu sana sio kama hawezi kusema laa hasha. Hivyo ameomba kumuelewesha kitu dada huyo ambaye anaonekana amejaa chuki na wivu juu yake.
“Kaa Lea mtoto wako. Na ujifunze jinsi ya kumtreat mwanaume ili usiwe unatuonyesha maisha yako ya chumbani na kutupostia maalama unayo dundwagwa ndani. Kiufupi Maisha nayo ishi hujawahi ishi usikae kujilinganisha na Mimi, chuki zako zilianza toka nimefungua ofisi mpaka ukawa unashirikiana na watu wangu wa karibu kuiua ofisi yangu ili nishuke tu.
“Kwa kifupi, kama unayapenda sana maisha yangu nakukaribisha na familia yako, maana Jumba ninalokaa ni kubwa sana na Location ni Mbezi Beach Karibu. Acha kunifuatilia mimi nikitrend wewe inakuhusu nini?. Mbona wewe ukitrend sijawahi kukukandia kua kiakili ushakua mama kazi kutrend kwenye meza za kidimbwi huna Future.
“Unaacha kutafakari jinsi ya kutengeneza tonge unakaa kuniandikia vijembe na kunikosoa. Mbona wewe ushachukuaga adi video za uchi na hakuna anae kubuguzi. Unikome na unitue kwenye Hilo domo lako Kama Buti la jeje,” ameandika Nai kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio