January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nadal kushiriki mashindano
ya tenis Monte Carlo Masters

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

NYOTA nambari moja wa zamani katika mchezo wa tenis duniani kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal amethibitisha kushiriki mashindano ya tenis ya Monte Carlo Masters mwezi ujao.

Wakiweza wazi hilo, waandalizi wa mashindano ya hayo wamesema, Mhispania huyo ambaye kwa sasa anashika namba tisa kwa ubora duniani anarejea kwenye mashindano hayo baada ya kupona jeraha la nyonga.

Bingwa huyo wa Grand Slam mara 22, hajacheza tangu kutetea ubingwa wake wa Australian Open baada ya kushindwa raundi ya pili na Mackenzie McDonald, kutokana na kupata jeraha.

Nadal alijiondoa kwenye mashindano ya Indian Wells na Miami mwezi huu lakini anatazamiwa kurudi kwenye Ziara ya ATP kwenye eneo analopenda zaidi baada ya kuongeza mazoezi katika wiki iliyopita.

“Rafa alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa,” mkurugenzi wa mashindano ya Monte Carlo David Massey amesema katika taarifa yake leo.

“Anataka kucheza Monaco na anajipa kila nafasi ya kuweza kushiriki katika michuano hii anayoipenda sana, ambayo ameshinda mara 11 kwa mchezaji mmoja mmoja, ikiwa ni pamoja na rekodi ya mataji manane mfululizo kati ya 2005 na 2012.”