Na Queen Lema Arusha
Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako Mkoani Arusha Nabii Dkt Geor Davie ametoa kiasi cha Milioni 100 kwa wafanyabiashara wa soko la samunge kwa ajili ya kuendeleza biashara zao baada ya kukumbwa na janga la Moto miaka michache iliyopita.
Aidha mbali na Nabii huyo pia amehaidi kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara hao hasa pale watakapokuwa na mahitaji mbalimbali.
Akizungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza Jana katika eneo Hilo la Samunge,Nabii Geor Davie amesema kuwa huwa anaguswa Sana na maisha ya watu wa Chini Hasa wajasiriamli wadogo wadogo
“Nawaheshimu sana wajasiriamli hawa wadogo wadogo kwa kuwa huwa wanajinyima Sana Sana na kisha kufanya maendeleo Yao,na unaweza kukuta mtu ana mtaji wa elfu Kumi na tano na anajenga nyumba na mwingine analipwa mshahara hata Milioni lakini hafanyi Jambo la maana kwa maana hiyo Mimi huwa nawaeshimu na ndio maana Leo nimekuja kuwatia Moto kidogo”amesema.
Amesema kwa kusema mahitaji ni mengi sana kwenye jamii na kamwe Serikali haiwezi kumaliza maitaji hayo kwa pamoja Ila inahitaji nguvu ya pamoja ya kuweza kutatua maitaji hayo.
Amesema kuwa huu ni wakati sahihi sasa wa Viongozi wa dini kuhakikisha kuwa wanakuwa sehemu ya faraja kwa kuweza kuwasaidia wahitaji kwa kuwa nao hiyo hiyo jamii inachangia kuwapandisha viwango vya kimaisha.
“Jamani huu ni muda muafaka sasa wa kuweza kuwakumbuka hawa wahitaji nawakumbusha Tu hizi sadaka zao za Mia tano tano elfu moja moja zimechangia sana kutupandisha mpaka hapa tulipofika kwa sasa kwa hiyo tuwasaidie na Sisi na hapo tutapata baraka Tele,”amesema na kuongeza
Na hapa Nilikuwa nimekuja na mfano wa hundi ya Milioni 50 lakini kweli nimeguswa Sana Sana naomba niongeze na sasa nitawapa kiasi cha Milioni 100 nitakabidhi kwa kuweza katika akaunti yenu na Nina tamani Sana mkaongezeke zaidi na zaidi”amesema.
Awali mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo amesema kuwa Kiongozi huyo wa kiimanj anatakiwa kuigwa kwa kuwa amekuwa faraja hasa kwa wale ambao ni wahitaji bila kuangalia Jambo lolote lile
Gambo amesema kuwa kwa kuangalia huko wahitaji kumempelekea kuweza kugusa mioyo ya wafanyabiashara mbalimbali wa Soko la samunge ambao hapo waliunguliwa na Soko mwaka 2019.
Kutokana na hilo,Gambo amesema kuwa na yeye kama mbunge wa Jimbo arahakikisha kuwa anakuwa msemaji wa Soko Hilo kwa kuishauri Jiji la Arusha kuweza kutatua changamoto ambazo zimo ndani ya Soko hilo.
“Bado kuna changamoto hapa sokoni kama vile ukosefu wa mageti ya uhakika,pamoja na ukosefu wa mitaro Ila Mimi natangaza kuwa nitatoa kiasi cha Milioni 10 kwa ajili kutatua changamoto hiyo”ameongeza Gambo
Nao wafanyabiashara wa Soko hilo wamemshukuru Nabii huyo ambaye pia ni Balozi wa Amani kwa kuweza kuwasaidia mitaji.
Wamesema toka kuingia kwa Soko hilo wamekuwa wakiyumba kwa kuwa walipoteza rasilimali ambayo ni muhimu kama vile mitaji lakini sasa kupitia msaada huo wataweza kunyanyuka na hivyo wataupiga Vita umaskini.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua