December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwezi Mtukufu wamuibua Nai, awafunda Harmonize, Rayvanny

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

VIDEO Vixen matata na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nairath Ramadhani maarufu kama ‘Official Nai’ amewataka Wasanii wenzake Rajabu Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ Bosi wa Kondegang na Rayvanny Bosi wa Next Level Music, kuacha mambo ya bifu na kufanya mambo yanayompendeza Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akitoa ujumbe huo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Nai amesema,
wasanii ni kioo cha jamii ni vyema kufanya mambo yanayo wapendeza Mashabiki kuliko kulumbana kwa mambo yasiyo na msingi katika mitandao ya kijamii.

“Mungu ni mwenye huruma sana na sisi waja wake. Tunatenda zambi nyingi sana, tunamkasirisha sana lakini kwa mapenzi yake ameweka msamaha na ukimuomba anakusamehe. Nmejiuliza sana kwanini sisi Binadamu hatuwezi kusamehe, kwa nini tunapenda Vita?. Ifikie wakati tumuogope sana Mungu laiti kama angekua anatuhukumu kwa makosa sijui kama tungefika leo.

“Tuishi kwa upendo, tuacheni chuki, maisha ni mafupi sana na maisha tunategemeana. Mimi kama mimi ninafunga na kukemea Shetani alie tutawala kwenye Industry Yetu, Inshaalah. Harmonize, wewe ni Muislam na hii ni Ramadhani, Utumie muda huu vizuri kusali na kumuomba sana Mungu. Rayvanny unafahamu maisha ni mafupi, ishi maisha yako, pambania Riziki yako na kazi zako,” ameandika Nai.

Hata hivyo, Nai amemuomba Mwenyezi Mungu awabariki wote na wale walio husishwa kwa mujibu. anwapemda sana wote. Mungu awasafishe nyoyo zenu. Ramadhani Kareem. Tanzania yetu ya Amani